Skip to content
Advertisements

WABONGO WAMKWAZA LULU DIVA KIMAPENZI

HIT maker wa Kibao cha Usimwache, Lulu Abasi maarufu kama Lulu Diva, ameelezea kukwazwa kwake na wanaume wa Kibongo kutokana na utapeli wao wa kimapenzi, tofauti na wenzao wa mataifa ya nje.

Bila kufafanua mataifa ambayo wanaume wake siyo matapeli wa kimapenzi, Lulu Diva aliiambia Risasi Vibes kuwa amefuatilia mahusiano mbalimbali ya kimapenzi na kugundua kuwa wanaume wa Tanzania ni waongo na matapeli wakubwa kwenye suala la uhusiano.

“Wanaume wa Bongo ni waongo usipime, nimefuatilia mahusiano kibao nchini, wanawake wengi wanalia kwa kudanganywa, maisha yao yanabadilika na kuvurugika na wanapoteza dira kwa sababu tu ya utapeli, tofauti kabisa na nchi zingine, kwa kweli wana haja ya kubadilika” alisema Lulu.

Advertisements
%d bloggers like this: