Skip to content
Advertisements

Warushiwa kichwa cha nguruwe

Familia moja ya waislamu mjini Manchester imetipoti kurushiwa kichwa cha nguruwe katika nyumba yao na mtu asiyejulikana.
Kwa mujibu wa habari,familia hiyo ghafla iliskia kioo cha nyumba kimevunjwa na tofali na muda si mrefu kichwa cha nguruwe kikarushwa.
Waislamu katika jengo hilo wamelalamika kuvamiwa namna hiyo na mtu asiyejulikana.
Hata hivyo ripoti zinaonyesha kuwa aliyerusha tofali na kichwa kile ni kijana wa miaka 18 aliyekuwa amejifunika uso.
Kijana huyo alifanya shambulizi hilo na kisha akapanda gari na kutokomea.
Polisi wanaendeleza uchunguzi zaidi.

Advertisements
%d bloggers like this: