Skip to content
Advertisements

Simulizi ya “Regret ” Sehemu ya pili 

“Kama ni kumsaliti baba basi kamsaliti na kama ni kutaka kumfilisi,atafanikiwa kama baba hatapata ukweli juu ya tabia za ma mdogo,
Hivi baba anavyo mpenda huyu mwanamke nikimwambia atanikubalia? Au ataenda kumwambia ma mdogo,maana

huwa nawasikia watu wakisutana mitaani kuwa wewe unaongea na mpenzi wangu ukiwa umevaa nguo na mimi ninaongea nikiwa kama nilivyo zaliwa je nani wa kusikilizwa..?,haaa nitachemka ila itanibidi nitumie njia mbadala”

yalikuwa ni mawazo baada ya kushuudia ma mdogo mke wa baba yake akitoka kimapenzi na msomba maji tena bila aibu.
“Sikia baby usiwaze kuhusu huyu kahaba kwani namhudumia mwenyewe na hata baba yake kajaa kiganjani kwani wala haongei na hakohoi kwangu kadata kweli kweli yani ninacho taka ndo anacho kifanya cha msingi nipatie kile roho yangu Inapenda si unajua nakupendea nini…” 

 Walifanya kupeana hizo roho zao kama walivyo ahidiana mpaka ikawa kero kwa makelele aliyokuwa anayatoa mama kwa sauti ya juu sana na hata mlango wao hawakuufunga bali walisogeza kidogo na kuachia upenyo ambao uliniumiza akili,kwakuwa ulipitisha zile sauti za mahaba niuwe sawia yani kama ma mdogo alikua akifanya makusudi kwani si kwa sauti ile alikua akihema kimahaba Sikupata kabisa usingizi mana ilifkka paka kipindi na mimi hisia za kufanya ngono zilinijia nami nikatamani sana kufanya tendo lile,

 Lakini Nilipata sana asila kwa tabia ile chafu ya ma mdogo,,

Kulipambazuka kwa namna yake kwani nilikuta mlango wa chumba cha baba ukiwa wazi na kuwakuta muuza maji na ma mdogo wamelaliana tena wakikoroma na wakiwa uchi kama walivyo zaliwa.Chini ya kitanda niliona Chupa za pombe aina ya kilimajaro sakafuni bila aibu wala kupepesa macho nilichukua shuka ambalo lilikuwa chini ya kitanda likiwa linanuka uvundo wa pombe na kuwafunika hivyo hivyo.
Yalipita masaa kazaa na hali ya hewa ikaanza kubadilika baada ya jua kuanza kuongeza joto la hali ya juu utazani tuko Dar kumbe tuko Mbeya city.
Baada ya hapo ata sikujua nini kimenipata kwani Nilishangaa pale nilipo jilazimisha kukaa ikawa ngumu na nikajinyanyua tena lakini nilirudi kitandani,

nilipojilazimisha zaidi ndipo nilipo hisi maumivu makali mgongoni kwangu.Na nilipo fumbua macho,nilimuona mama cather akiwa kando yangu na sikuona tabu kumuuliza

“Ma cather kulikoni,mmenileta hapa? Na ma mdogo yuko wapi? Na vipi kuhusu msomba maji?…?” Nilifululizia maswali mpaka nikawa najishangaa kwani hata yeye hakuamini,bali alionesha tabasam la kunituliza na kunifariji na nilimshangaa kwa sikujua Nimefikaje pale na nilikua na maumivu mwili mzima nilikua nikihisi kufa kufa tu__
Lakini Mama cather hajawahi kuwa karibu na mimi na hata familia yetu zaidi ya kuwa majirani na kupeana salamu tu,
“Mwanangu kwanza pole na ulipo hapa ni hospital ya Bugando,Nimekuleta hapa kutokana na ajali uliyoipata na yapata siku nne na leo ya tano ndo umezinduka”

 Nilishangaa sana nilipoteza fahamu,sikuelewa kilicho endelea mpaka nakuja kuzinduka,najikuta nyumbani kwa Ma cather.Nilikuwa nimefungwa bandage ngumu mkononi na kichwani nilikuwa nimezungushiwa kitambaa aina ya gozi.Kwa haraka nikagundua kweli nimepata ajari lakini sikutambua ni ya aina gani maana sikuwahi kwenda barabarani.

“shikamooooh!!,ma cather?” Nilimsalimia baada ya kumuona akija kitandani kwangu “Marahaba mwanangu,unaendeleaje lakini” Niko salama mama,Lakini naomba nikuulize kitu mama cather
 “Uliza tu nakusikiliza lakini,kwanini usinywe chai kwanza ili uweze kupata nguvu mwilini?? 

Ma cather alinishauri na mie Nilijikokota japo kwa shida mpaka sehemu ya sinki la kunawia na nikanawa

“unaonekana huamini kilicho tokea mpaka sasa unavyo jitizama eeeh…??” Ni swali ambalo lilinigusa sana na kuamsha maswali yangu ya kutaka kufahamu lilicho nisibu.”ndio mama maana hata sijitambui kabisa na ninapotaka kuvuta kumbu kumbu kichwa kinaniuma sana na sielewi kitu,yani sijui ata nimekuaje??

Mama cather alinyenyuka na kutoka nj’e

Mara mlango ulifunguka na nikakutana uso kwa uso na sura ya baba angu na sikuamini kwani alionekana nimtu ambae ametoka kulia mda si mrefu.

“kulikoni baba…? Mbona unaonekana kama ulikuwa unalia??” Aliniangalia na kisha kunikumbatia uku akilia
“kwani baba nimepatwa na nini?Na wewe umerudi Lini?Mbona mi sielewi Mpaka leo niko mlemavu wa mkono?” Baba akajishika kichwa

 “Nisamehe mwanangu,me ndo mwenye makosa na ndie niliesababisha ajali yako,wala haikuwa makusudi bali ni bahati mbaya”..Nilizidi ujawa na ukungu ndani ya ubongo na kukosa ushirikiano kati ya akili na masikio,sikuona tabu kuendelea kwa ishara tu kumruhusu baba aendele kunisimulia Kiilicho nipata.
Baba alianza kunisimulia…
“Unajua siku nyingi sana wakati wewe ukiwa shule,hukuwahi kuonana na mama yako na kama ukija kuonana nae sidhani kama utaweza kumtambua Kwani bajua aliondoka ukiwa mdogo Na mpaka leo ninavyo kueleza alitoweka na wanangu yaani wadogo zako mapacha waliitwa Janeth na josia.Ambao ni kurwa na dotto Nilimpenda sana mama yako yani hat zaidi ya neno sana sikupanga niachane nae wala kumuacha ila aliamua kuondoka mwenyewe kisa alihisi mi natembea na mfanyakazi dada wa kazi(house Girl) ambae ndo Mama yako mdogo kwa Sasa na ndo ulikua ukiishi nae” Nilimstopisha baba asiendelee, 
Na mimi nikauliza “Kwani mama yangu yuko wapi? Na wadogo zangu wako wapi pia? Na mama angu aliitwa nani? ” baba alishusha pumzi iliyonipa hofu.Na hofu hiyo ikanifanya nikae sawia kusikiliza kwa umakini 

“Najua unahamu ya kufahamu yuko wapi mama yako na wadogo zako.Bali sikilisa kwa umakini,Kipindi hicho nilikuwa natoka safari katika bishara zangu kama unavyo jua biashara zangu nafanyia uko naweza hata kukaa miezi 3 au 2 nikiwai sana ni mwezi 1 Lakni siku hiyo, Nilipofika nyumbani bahati mbaya ama nzuri sikufanikiwa kumkuta Mama yako wala wanangu.Nilicho ambulia ni kukutana na ujumbe ambao aliuandika mama yako na akiwa kaambatanisha na vipande vya picha,

Mara Gafla Baba akaanza kulia na kufanya Ma cather na Mume wake kuingia katika kile chumba na kumkuta Baba akilia kwa sauti kubwa sana huku kapiga magoti kuashiria kuomba msamaha…”vipi mwenzetu kulikoni? Kwanini unalia kwa sauti sio vyema mzee mwenzangu” yale maneno yakawa yamempunguzia uchungu aliokuwa nao baba.”Ndugu zangu kwanza niwashukuru kwa huduma mlizompatia mwanangu kipenzi,sina cha kuwalipa zaidi ya Mungu ndo anajua.Na tatizo linalo niliza ni kuhusu mke wangu.”kabla ajamalizia kuelezea ma cather alidandia maneno “haa…yule kahaba..bado unamuhitaji tuuu??..umekuwa sasa achana na wanawake wasio na faida kwako”

Baba akajibu..

” hapana nilikuwa namaanisha mama yake na Samia,lakini tatizo ni kile kitu nilichomfanyia mpaka akaondoka kwangu nahisi ni mkosefu kwake na hata sielewi aliko elekea yapata miaka 7 sasa”

Me najua alipo mama Samia,ila naomba Mueleze kwanza Samia kilicho mkuta mpaka akawa hivyo na ya mama yake tutaongea baadae
“alidokeza ma cather kisha wakatoka na mume wake wakiwa wamejawa na huzuni

Tulibakia wawili me na baba tukawa tunapishana macho,nikimwangalia yeye anatizama chini.Sikuelewa nini tatizo bali nilijipa ujasiri “hivi baba kumbe Ma mdogo alikuwa changu doa na ukaamua kabisa kujimilikisha?
Itaendelea..

Mtunzi: D’ mark Mgoba 

Mwandishi: Azizi Ally

Advertisements
%d bloggers like this: