Skip to content
Advertisements

LIL WAYNE KWENYE HEADLINES TENA! KWENYE HILI HACHOMOKI

Lil Wayne anaweza kuwa Baba wa mtoto wa miaka 15, ila alikuwa hafahamu!

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa, Mwanamke mmoja amejitokeza na kudai kuwa rapa #LilWayne ni baba mtoto wake, ambaye ni kijana mwenye Umri wa miaka 15 sasa.
Mwanamke huyo, Keiotia Watson, ameibuka na nyaraka halali akidai aliwahi kukutana na Lil Wayne kimwili..! Ilikuwa June mwaka 2001. Na miezi 9 baadae (February 2002) alijifungua mtoto wa kiume ambaye alipewa jina la DWAYNE, ambalo jina kamili la Lil Wayne.

Keiotia Watson,


Watson pia amefunguka kuwa juhudi zake za kufika Mahakamani kupatana na Wayne ili kupata (Child Support) ziligonga mwamba mara kadhaa, kwa Mahakama kushindwa kumpata.
Chanzo cha karibu na rapa huyo mzaliwa wa New Orleans Louisiana, kimesema kuwa, Wayne yupo tayari kufanya vipimo (Paternity Test) na kama ikithibitika ni kweli, basi atachukua Majukumu yote juu ya mtoto huyo.
Wayne tayari ana watoto wanne, na kila mmoja akiwa na Mama yake.

Kulia ni kijana inaye semekana ni mtoto wa Mwanamziki Lily wayne

Advertisements
%d bloggers like this: