Skip to content
Advertisements

MADEE: SIAMINI KAMA ROMA ALIKWENDA ZIMBABWE

Kushoto “Roma Mkatoliki” Kulia “Madee”

MSANII wa Bongo Fleva, Ahmadi Alli ‘Madee’ anayefanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘Sema’ ametoa povu juu ya wimbo wa Roma Mkatoliki wa ‘Zimbabwe’ akisema ni mzuri ila haamini kama kweli alienda nchini Zimbabwe kama alivyodai wakati wimbo huo unatoka.

 

Ameyasema hayo katika kituo kimoja cha radio hapa nchini kuwa kituo cha radio kilijaribu kumhoji Roma mambo kadhaa lakini hakuwa na majibu yenye ushawishi, kitu ambacho kinamfanya kutoamini juu ya safari hiyo.

 

“Tulijaribu kumhoji juu ya uwanja wa ndege wa Zimbabwe unaitwaje akaingia chocho, hajatutajia hadi leo. Kwa hiyo ni muongo, muongo sana lakini wimbo wake ni mkali kinoma ila yeye simuamini hata kidogo,” alisema Madee na kuongeza:

 

“Ila la Zimbabwe siliamini, hilo la kutekwa muache mwenyewe, inaweza kuwa kweli au si kweli. Kuna kitu kimoja ananichanganya, yeye kaumia mkono halafu eti anachechemea si uongo huu?” alisema Madee.

 

Hata hivyo, amesema kuwa muda mwingi yeye na Roma huwa wanapiga stori za kifamilia na utani mwingi, na watu wanapoona kitu chochote kwenye mitandao kati yao wasikichukulie kama kweli kwani huwa ni utani.

Advertisements
%d bloggers like this: