Skip to content
Advertisements

Wasiojulikana wafanya mauaji Zanzibar

Mtoto mwenye umri wa miezi kumi Arman Hassan Mohamedi, ameuawa na watu wasiojulikana katika eneo la Fuoni lililopo mkoa wa Mjini Magharibi Unguja visiwani Zanzibar, na kisha kumtumia ujumbe mama mzazi wa mtoto huyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Maghari Unguja, Hassan Nasir, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 3, ambapo mtoto huyo aliuawa na kisha kutumbukizwa kwenye dumu la maji la lita 60, na kulitelekeza nyumbani kwao.
“Upelelezi wa awali unaonyesha aliuawa na mtu ambaye hajafahamika bado, tunasema ameuwawa kwa sababu alikuwa alikuwa nje na watoto wenzake wakicheza, baada ya muda akatoweka, akatafutwa sehemu mbali mbali hadi vituo vya polisi, lakini kwenye saa moja na nusu akaonekana akiwa kwenye dumu la maji la lita 60 akiwa ndani amekufa, lakini kuna message alitumiwa mama wa mtoto kwamba mtoto wako atapatikana akiwa maiti, na nyingine ikimpa pole kwa msiba”, amesema Kamanda Nassir

Kamanda Nassir amesema Jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuchunguza kwa kufuatilia messgae hizo ili kuwabaini waliofanya mauaji hayo, aliyoyaita ya kikatili na kuwachukulia sheria stahiki.

Advertisements
%d bloggers like this: