Skip to content
Advertisements

Siri yafichuka kuhusu Alikiba na Jokate

Joketi Mwegelo

Mahusiano kati ya msanii Alikiba na aliyeaminika kuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo, ambaye ni mwanamitindo na mjasiriamali anayetazamwa na dunia nzima, bado yanaendelea kwa upande wa kazi za sanaa, ambapo wawili hao ni mtu na bosi wake. 

Siri hiyo imetolewa na msanii Abby Skills ambaye pia ni mtu wa karibu na Alikiba na moja ya msanii ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Alikiba, alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kusema kwamba Jokate yupo chini lebo ya Alikiba, ambayo pia yeye yupo.
“Mimi pia nipo chini ya lebo yake, Alikiba ni bosi wangu, kuna Abdu Kiba, kuna Salim, kuna Heri, kuna Jojo Jokate”, amesikika Abby Skills akitoa siri hiyo ambayo hakutakiwa kuiweka wazi kwa mujibu wake mwenyewe. 
Alikiba na Jokate waliwahi kuwa na tetesi kuwa na mahusiano ya kimapenzi, na hivi karibuni Alikiba alisikika akisema hadharani kwamba hana mahusiano na mwanamitindo huyo.

Advertisements
%d bloggers like this: