Skip to content
Advertisements

Madee kaitosa rasmi Arsenal

Mkali wa Bongofleva anaeiwakilisha TipTop Madee ameitosa hadharani Arsenal na kutangaza kuanzia sasa yeye ni shabiki wa Njombe Mji ya mkoani Njombe inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara. 

Akiwa kwenye jukwaa la Fiesta 2017 ndani ya ardhi ya Njombe, Madee anayefahamika kuwa ni shabiki wa kutupwa The Gurners aliikacha na kujitangaza kuwa yeye anai-support Njombe Mji. 
“Mimi bwana Simba, sipo Yanga, sipo Manchester wala Arsena, mimi ni Njombe Mji (akavua koti kubwa alilokuwa amevaa na kubaki akiwa na hezi ya Njombe Mji).” 
Mbali na hayo yote Madee alichukua mpira akapia danadana kadhaa kisha akaupiga kwa mashabiki waliofurika uwanja wa Sabasaba kwa ajili ya burudani ya Fiesta.

Advertisements
%d bloggers like this: