Skip to content
Advertisements

Waliopitiwa na Panga la Rais Magufuli Baraza la Mawaziri.

Ni mara ya kwanza kwa rais Magufuli kufanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la Mawaziri.

Mapema mwaka huu Rais Magufuli alifanya mabadiliko katika wizara ya habari na kumuondoa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye na kumteua Dk Harison Mwakyembe
Panga jipya la Rais Dk Magufuli limempitia Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Thomas Kashillilah ambaye nafasi yake imechukuliwa na Steven Kagaigai
Rais Dk Magufuli amesema kuwa Dk Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine.
Mawaziri waliotupwa nje ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.
Katika panga pangua ya Rais Dk Magufuli, mwingine aliyetupwa nje ni aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi, Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye panga hilo limepita na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.
Rais Magufuli amewataka wale walioteuliwa katika nafasi hizo kama watakuwa wamezipokea Jumatatu atafanya shughuli ya kuwaapisha wateule hao.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: