Skip to content
Advertisements

Wasiojulikana wamuua producer

Producer maarufu nchini uganda Danz Kumapeesa amefariki dunia baada ya kukaa hospital kwa muda mrefu akitetea uhai wake, tangu alipovamiwa na watu ambao bado hajajulikana mpaka sasa na kuumizwa kikatili miezi miwili iliyopita.

Danz amefariki asubuhi ya leo kwenye hospitali aliyokuwa akitibiwa majeraha aliyoyoyapata kichwani kwa kipigo alichopewa na watu wasiojulikana, alipokuwa akitokea kwenye mizunguko yake na kupelekea kulazwa hospitali ya Nsyamba.

Danz Kumapeesa atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki wa Uganda, kwa kufanya kazi na wasanii wengi maarufu kama Eddy Kenzo, Irene Ntale, Bebe Cool na Sauti Sol.

Kazi ya mwisho kwa msanii huyo ‘Mbozi za Malwa’ aliyofanya na wasanii Bebe Cool na Sauti Sol, inaendelea kufanya vizuri kwenye media nyingi Afrika Mashariki na kati.

Advertisements
%d bloggers like this: