Skip to content
Advertisements

17 wafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ubakaji

Jeshi ka polisi mkoani Mtwara limewafikisha mahakamani watu 17 kwa tuhuma za makosa ya ubakaji pamoja na kuwapa mimba wanafunzi, katika kipindi cha miezi miwili kuanzia Julai mpaka Septemba mwaka huu. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, amesema bado jeshi hilo linaendelea kufanya msako wa watuhumiwa wengine 82 wanaodaiwa kuhusika na makosa ya uzalilishaji kwa wanawake na watoto wakike yakiwamo ya ubakaji na kuwapa mimba wanafunzi. 
Aidha, katika hatua nyingine amesema kwamba mtandao wa kijambazi umeingia mkoani Mtwara kutoka baadhi ya mikoa hapa nchini, na kufanya tukio moja la kihalifu kwa kumvamia, kumjeruhi na kisha kumpora fedha mfanyabiashara Shafih Bakari, kiasi cha shilingi Milioni Moja akiwa nyumbani kwake. 
Amesema kwamba katika tukio hilo mfanyabiashara Bakari ameporwa vocha zenye thamani ya shilingi Milioni tano na tayari wanawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuhusika.

Advertisements
%d bloggers like this: