Skip to content
Advertisements

Shamsa Ford afunguka baada ya mume wake kuchepuka

Muigizaji wa filamu bongo Shamsa Ford ambaye ni mke wa mfanyabiashara wa mavazi Rashid maarufu kwa jina la Chid Mapenzi, amewajia juu wanaoingilia kati ndoa yake baada ya tetesi za mume wake kuchepuka, wakimtaka kuchukua hatua kwa haraka na kumuacha. 

Kwenye ukurasa wake wa instagram, Shamsa ameandika ujumbe akieleza ni kiasi gani anampenda mume wake huyo na kumfurahia pale anapoomba msamaha akikosea, huku akisema hatokuja kumuacha mume wake hata kama amemsaliti. 
“Mume wangu nikikuelewa mimi inatosha wengine wakipiga kelele tuchukulie kama burudani tu, jamani sitokuja kumuacha mume wangu kwa ajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamiii. Amecheat Bili Clinton sembuse Rashid wangu”, ameandika Shamsa. 
Hivi karibuni shamsa aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram, akisema kwamba anaona kuna ‘jini mkata kamba’ anainyemelea ndoa yake, na ndipo zilipofuatia taarifa za mume wake kusaliti ndoa na kuwa na mchepuko. 

Nakupenda mume wangu halali wa ndoa aliyenipa Mwenyezi Mungu.Sitoachana na wewe kwa ajili ya makelele ya wanadamu nitaachana na wewe kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu..Unanipenda,unaniheshimu, unajishusha kuomba msamaha pale unapokosea wakati wanaume wengine hawawezi kuomba msamaha hata wakikosea. Mume wangu nikikuelewa Mimi inatosha wengine wakipiga kelele tuchukulie kama burudani tu.Maana anajitahidi huyo anayeitwa ILALA MJINGA kama ulivyomsave kwenye simu yako kusambaza msg kwenye magroup na kuwatumia waandishi ushahidi..jamani sitokuja kumuacha mume wangu kwa ajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamiii. Amecheat Bili clinton sembuse Rashid wangu ? Nakupenda RASHID WA SHAMSA FORD tupambane tuzidi kujenga familia yetu..

A post shared by Shamsaford (@shamsaford) on

Advertisements
%d bloggers like this: