Skip to content
Advertisements

DOGO JANJA AMZIMIA VEE MONEY

MKALI wa Ngoma ya Ngarenaro, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, amefunguka kuwa hakuna mwanamuziki wa kike Bongo anayemzimia kama Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kutokana na swagga zake.

Dogo Janja ambaye amekuwa akihusishwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Uwoya madai ambayo ameyakana na kudai yeye ana mwanamke wake ambaye hayupo kabisa kwenye sanaa aliongeza kuwa, Vee humkosha zaidi na wakati mwingine anatamani mastaa wa kike Bongo wangekuwa wanavaa kama yeye.

“Kiukweli huwa nazimia sana swagga za Vee Money, anajua kupendeza na kuna wakati huwa natamani mastaa wa kike wote wavae na kutupia pamba kama yeye,” alisema Dogo Janja.

Advertisements
%d bloggers like this: