Skip to content
Advertisements

Wema;Soudy kwani huna mama wa kumfanyia hivyo?

Mwigizaji kutoka kiwanda cha bongo movie wema sepetu amemjia juu mtangazaji wa kipindi cha shilawadu Soudy kwa kitendo cha kumpigia mama yake simu na kuanza kumuuliza kuhusu ugomvi wa wake na dada yake Diamond platnumz “Queen Darlin ” ambao inasemekana ulitokea siku ya birthday party ya Diamond ambapo wema alialikwa na kwenda.

Mama wema alipopigiwa simu hakupenda kile kitendo na kumwambia Soudy kuwa Wema ni mtu mzima hupaswi kuniuliza mimi mambo yake.

Wema pia ameonyesha wazi kukasilishwa na kitendo cha Soudy kurusha hewani record za mama ake huku maneno mengine yaliyo recodiwa yakiwa makali kidogo.

Kupitia kurasa wake wa Instagram wema aliweka wazi hisia zake kwenye tukio hilo na kuonyesha kukerwa.

Advertisements
%d bloggers like this: