Skip to content
Advertisements

Mwanafunzi auwawa kwa mawe na wananchi wenye asira kali

Mwanafunzi anayetuhumiwa kuhusika na shambulizi lililogharimu maisha ya watu 6 katika shule ya Bweni kaskazini mwa Kenya ameuawa baada ya kushambuliwa kwa mawe na wenyeji waliokuwa na hasira,maafisa wamethibitisha. 

Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa amesimamishwa kuendelea na masomo huko Lokichogio alitiwa nguvuni kabla ya wananchi waliokuwa na hasira kuvamia kituo cha polisi na kumtoa mahabusu. 
Kwa mujibu wa Seif Matata kamishna wa kaunti ya Turkana Mwanafunzi huyo alikamatwa baada shambulizi shuleni hapo kusababisha vifo vya watu sita watano kati yao wanafunzi na mlinzi mmoja. 
Nao mashuhuda wameeleza kuwa watu watatu waliokuwa na silaha, miongoni mwao aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo walivamia mabweni katika Shule ya Upili ya Lokichogio jumamosi. 
Lokochogio imepakana na Sudan Kusini na Ethiopia na wenyeji wa eneo hilo mara kadhaa hubeba bunduki kwa ulinzi wa mifugo yao.

Advertisements
%d bloggers like this: