Skip to content
Advertisements

Msako wa mchawi Zambia

Msako wa mchawi umepelekea kituo cha polisi kucomwa moto nchini Zambia.
Kwa mujibu wa habari, wakazi wa wilaya ya Mufumbwe walikusanyika barabarani na mitaani wakiwa wamebeba jeneza wakidai kumsaka mchawi aliyembaka na kumuua mtoto wa shule.
Kundi hilo la watu lilibeba jeneza na kuzunguka wilaya nzima likimsaka mzee mmoja kwa madai ya kuwa amembaka na kumuua mwanafunzi kwa kutumia uchawi.
Polisi walipojaribu kutuliza ghasia hizo,walivamiwa na kuzidiwa nguvu na wakazi hao hali iliyowafanya mapolisi hao kurudi katika kituo cha polisi.
Ripoti zinaonyesha kuwa kundi la watu hao wenye hasira waliwsha na kukichoma moto kituo hicho,hali iliyosabaisha maafisa polisi sita kujeruhiwa.
Ni tamaduni ya wakazi wa Zambia kubeba jeneza wakati wakimsaka mchawi.

Advertisements
%d bloggers like this: