Skip to content
Advertisements

MILLEN MAGESEWA AIKUMBUKA SIKU YA MAAJABU YA MTOTO WAKE WA KWANZA MAISHANI

Mwanamitindo wa kimataifa maarufu kutoka Tanzania anayeishi Marekani, Happiness Magese ‘Millen Magese’ Baada ya kutafuta mtoto kwa kipindi kirefu, furaha yake imeendelea kuongezeka ukubwa huku akizidi kuikumbuka siku yake ya mafanikio na maamuzi magumu yaliyozaa matunda ya kupata mtoto wake wa kwanza.

Millen Magese ambaye mwaka huu alifanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza wa kiume aitwae Prince Kairo ambaye imehesabika kuwa ametimiza mwize 13 tangu azaliwe na leo kupitia ukurasa wake wa InstagramMillen ameusherehekea mwaka wa kumbukumbu ya siku aliyofanyiwa hatua za kufanyika kwa utungaji wa mtoto wake huyo nje ya kizazi (IVF).

Happiness Millen Magese ni shujaa kati ya mashujaa wakike Afrika aliyepigana vita kubwa ya tatizo la kiafya la seli zinazofaa kuwa ndani ya mji wa uzazi kuwa nje ya mji wa uzazi linalofahamika kitaalamu kwa jina Unaomdhoofisha ‘Endometriosis’.


Hata hivyo Millen Magese akiwa kama Balozi wa akina mama wote wanaopaitia tatizo la namna yake katika siku hii ya kumbukumbu ya maamuzi yake magumu ameendelea kuhamasisha akina mama kuwa wenye ujasiri na kuomgeza matumaini kuwa kama iliwezekana kwake pia inawezekana kwa mwingine.

Advertisements
%d bloggers like this: