Skip to content
Advertisements

Nakumatt Mlimani City yafungiwa

Uongozi wa Mlimani City umelifungia duka kubwa (supermarket) ya Nakumatt iliyopo eno hilo jijini Dar es salaam, baada ya kukosa bidhaa za kutosha kwa muda mrefu na kudaiwa kodi za huduma mbalimbali.
Taarifa ya kufungiwa huko imetolewa leo na Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastory Mroso na kusema kwamba kabla ya kufungiwa walishapewa notisi miezi minne kufanyia marekebisho tatizo hilo, lakini hakuna hatuo yoyote walioichukua, na kisha kuwapa tena notisi ya mwisho ya siku kumi ambayo ilikuwa inaisha siku ya Jumamosi, na kuamua kuwafungia asubuhi ya leo.

Pastory Mroso ameendelea kwa kusema kwamba tatizo hilo limekuwa likiwaathiri wafanyakazi na hata bidhaa za wafanyabiashara wengine, na pia wamelishalitolea taarifa serikalini kwa hatua zingine zaidi.

Advertisements
%d bloggers like this: