Skip to content
Advertisements

Ray C ampa onyo Nandy kuimba nyimbo zake Fiesta, ‘…Sijafa bado…

Msanii mkongwe wa nyimbo za Bongo Fleva, Ray C amemjia juu msanii mwenzake Nandy ambaye ameingia kwenye muziki siku za karibuni na kuonesha kufanya vizuri katika muziki wake.

Nandy ni kati ya wasanii wanaotumbuiza katika misimu ya Fiesta, na katika kutumbuiza kwake amekuwa akifanya baadhi ya nyimbo zake chache na za mwanadada msanii mkongwe Ray C.

Ray C ameonyeshwa kutokufurahishi msanii huyo kutumia nyimbo zake hali ya kuwa yeye bado yupo na angeweza kunufaika kupitia nyimbo zake kama zinapendwa hadi wengine kuzitumia katika maonyesho.

Kupitia kurasa wake wa intsagram Ray C ameandika waraka kwa Nandy, kuonesha hafurahishwi na kitendo chake cha kutumbuiza nyimbo zake ilihali yeye yupo hai.

Alichooandika Ray C, kupitia kurasa wake wa instagram.

‘Jamaani hii tabia sio nzuri kabisa!!! Sijafa bado! Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye show zenu muwe mnaniitaga basi! sina cancer ya koo ya kushindwa kuziimba hizo nyimbo! Nandy hii mara ya mwisho ukipanda fanya kazi zako! Hii mara ya pili ujue! Mashabiki zangu hamuwatendei haki! i don’t like it sipendi! Maana hata tukigongana muda mwingine hata salam hamnipi kwahiyo staki mazoea…….

“Niliimba tusitaftiane visa tena Pisha sio tena Presha”😬😬”.

Advertisements
%d bloggers like this: