Skip to content
Advertisements

ALIYEDAIWA KUBEBA MIMBA YA KIBA AFUNGUKA LIVE

Msanii Ali kiba

DAR ES SALAAM: BAADA ya picha na habari kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba ana ujauzito wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, mrembo Caroline Joseph amefunguka na kueleza anavyotishiwa maisha.

Akielezea sakata hilo ‘lililokiki’ mitandaoni wiki hii, Caroline alisema alishtushwa na taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba ana ujauzito wa Kiba jambo ambalo si la kweli kwani hajawahi kuwa na uhusiano naye na anamuheshimu kama kaka na ndugu yake.

“Sina mimba jamani na sina uhusiano na Kiba, kuna mtu amefungua akaunti feki kwa kutumia jina langu kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambaye anasema ana ujauzito wa Kiba na ameweka picha zangu eti na picha ya ultrasound ya mtoto tumboni na kusema Princes wa Kiba anakuja.

“Kiukweli nimeumia sana maana imenipa usumbufu hivyo nilienda kuripoti polisi katika kitengo cha makosa ya mtandao (Cyber Crimes) na wako kwenye uchunguzi wa kumpata huyo mtu anayetumia jina langu na kuweka picha zangu kunichafua ili achukuliwe hatua,” alisema Caroline.

Aidha, Caroline alieleza kuwa kutokana na sakata hilo amekuwa akipokea meseji za vitisho kwenye simu yake kwa namba ngeni kwamba watamfanyia kitu mbaya kwa kuwa anamchafua Kiba kwa kusema ana ujauzito wake.

“Nimepata vitisho kwenye simu yangu kwamba watanipoteza kwa kuwa ninamchafua Kiba lakini nimekuwa nikiwaambia waangalie kwenye Instagram mimi natumia jina la Dorothea-caroline9 lakini huyo aliyeweka picha na kusema ana mimba anatumia ambayo haina 9 mwisho na mimi sina wafuasi wengi ni mia saba tu.

“Nimeamua kwenda polisi ili huyo mtu akamatwe maana naweza kupata jambo baya wakati sina hatia yoyote, huyo mtu inawezekana anatafuta wafuasi kwa ajili ya kufanya biashara zake,” alisema Caroline.

Ili kuleta usawa wa habari, Risasi Jumamosi lilimtafuta Kiba kupitia kwa meneja wake, Aidan Seif hakupokea simu na hata alipotumiwa picha na maswali kuhusu habari hii kwa njia ya mtandao wa WhatsApp meseji zilionekana kumfikia na kuzisoma lakini hakujibu hata moja.

Kiba na Caroline waliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari baada ya picha zao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii wakiwa hotelini ambapo mwanadada huyo alifafanua kwamba alipiga picha kama shabiki wake tu.

Advertisements
%d bloggers like this: