Skip to content
Advertisements

HALI YA MBWANA SAMATTA NCHINI UBELGIJI YAZIDI KUWA MBAYA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza mechi ya tisa bila kufunga bao katika klabu yake, KRC Genk ingawa imeibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Anderlecht kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Constant Vanden Stock mjini Brusells.

Bao pekee la ushindi la Genk limefungwa na beki kinda wa umri wa miaka 22, Mghana Joseph Aidoo dakika ya 50 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mbelgiji, Siebe Schrijvers.

Samatta leo amecheza mechi ya 67 katika mashindano yote tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR

Katika mechi hizo, Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka jana alipokuwa na Mazembe, 39 ameanza na mechi 24 ametokea benchi, akifunga jumla ya mabao 21 kwenye mashindano yote.

Mara ya mwisho Samatta alifunga mabao mawili Genk Agosti 13, mwaka huu ikishinda 5-3 dhidi ya wenyeji, Royal Antwerp FC,

Advertisements
%d bloggers like this: