Skip to content
Advertisements

UMEINYAKA HII YA LULU DIVA KUMLILIA CHID BENZ?

HUKU wasanii mbalimbali wakimtaka rapa mkali Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, chipukizi anayefanya poa kwenye gemu la muziki, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ naye amemlilia, akisema kitendo chake cha kuendelea na ‘unga’ kinamuumiza.

Akipiga stori na Risasi Vibes, alisema jambo hilo linamuumiza kwa vile tangu akisoma alikuwa akifuatilia muziki wake, hivyo ni vyema kama angeachana na mambo hayo yasiyo na faida ili arejeshe heshima yake katika muziki.

“Namshauri Chid aachane na hayo mambo mengine, atulize akili yake kwenye muziki, naamini atafanya vizuri na kujiingizia kipato kizuri maana muziki wa sasa unalipa, ili ufanikiwe kwenye hii fani lazima utulize akili uipende na uipe heshima, akizingatia haya atarudi kwenye ubora wake,” alisema.

Advertisements
%d bloggers like this: