Skip to content
Advertisements

Chelsea yailaza Everton na kutinga robo fainali ya Carabao

Kaimu mkufunzi wa Everton David Unsworth amesema kuwa timu yake ilimfurahisha licha ya kutolewa katika mechi ya kuwania kombe la carabao dhidi ya Chelsea.

Willian alifunga bao muhimu la pili huku Chelsea wakisonga mbele na kuingia robo fainali lakini walishangazwa na wageni wao.

Chelsea ilikuwa imeitawala Everton kwa urahisi katika kipindi cha kwanza na kuongoza kupitia kichwa kizuri cha Antonio Rudigers.

Lakini The Toffees walionekana kuwa hatari baada ya kipindi cha kwanza huku shambulio la Kevin Mirallas likiokolewa naye Ademolar Lookman akipiga mwamba wa goli.

Willian alifunga bao la kimo cha nyoka katika dakika za lala salama kabla ya Dominic calvert kuifungia Everton bao la kufutia machozi.

Nilipotezavibaya lakini ninafurahia mchezo wetu, tuliwatawala,Unsworth aliyechukua mahala pake Ronald Koeman alisema.

Advertisements
%d bloggers like this: