Skip to content
Advertisements

LIL WAYNE ATISHIA KUIFUA YOUNG MONEY

Ni kweli huu unaweza ukawa ndio mwisho wa Young Money? Lil Wayne ametishia kuifuta kabisa lebo hiyo endapo Cash Money ya Birdman wameshindwa kuisimamia na kuiendesha vizuri.
Lil Wayne ametoa malalamiko yake kwa jaji pamoja na kutoa mapendekezo yake kuhusu lebo hiyo kupata mwendeshaji mzuri au kuifuta kabisa kama hatapatikana mtu huyo mapema. Wakati huo huo jaji ameombwa kusikiliza malalamiko jinsi ya ugawanywaji wa hisa za lebo hiyo.
Jaji pia amesikiliza upande wa Birdman ambaye anaendesha lebo hiyo chini ya Cash Money, amesema Lil Wayne hana haki za kufuta lebo hiyo akiwa chini ya Cash Money lakini kama akiwa nje ya Cash Money anaweza kufanya hivyo.
Ugomvi wa Lil Wayne na Birdman ulianza Disemba 2014, na ilipofika January 2015 bifu hilo lilipamba moto baada ya Wayne kutaka kulipwa kiasi cha dola milioni 51 kwa kuchelewesha kuachia albamu yake iliyotakiwa kutoka mwaka 2014.

Advertisements
%d bloggers like this: