Skip to content
Advertisements

USHAHIDI WA MKE WA DK SLAA KUHUSU UGONJWA WA KANUMBA UNAWEZA KUMSAIDIA LULU KWENYE KESI YAKE

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili staa wa filamu nchini, Elizabeth Michael Lulu leo Oktoba 25 imeingia siku ya nne mfululuzo katika mahakama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Siku ya jana, hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Sam Rumanyika, aliamuru afisa wa polisi aliyeandikisha maelezo ya shahidi muhimu wa upande wa utetezi, Bi. Josephine Mushumbusi, mke wa Dr Slaa yasomwe mahakamani sababu yeye hakuweza kufika mahakamani hapo kutokana na kuwa nje ya nchi.
Na sasa imefahamika kwamba kumbe, Bi. Josephine alikuwa pia ni daktari wa marehemu Kanumba.

Kwenye maelezo hayo yaliyosomwa na Detective Sergeant Nengea, Josephine alieleza, marehemu Kanumba alikuwa mmoja wa wateja wake kuanzia mwaka 2011 ambapo alienda kutoa sumu mwilini.
Maelezo yamedai kuwa marehemu alikuwa na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo na alikuwa anasikia maumivu katika ubongo huku pia akili kuchoka.
Detective Sergeant Nengea hakuulizwa swali lolote, ikiwa ni uamuzi wa jaji kwasababu yeye alikuwa mtu aliyeandika maelezo tu. Baada ya maelezo hayo kusomwa, Jiji Rumanyika amedai kuwa kesho, Oktoba 26, wazee wa baraza watakaa kujadili iwapo Lulu ana hatia yoyote katika kesi inayomkabili ya kumuua Steven Kanumba bila kukusudia.

Advertisements
%d bloggers like this: