Skip to content
Advertisements

SETH: MOBETO ALIJITABIRIA KABLA HAYAJATOKEA

MSANII wa filamu, Seth Bosco amefunguka kuwa sakata la kuzalishwa na kutelekezwa na msanii wa Bongo Fleva, mwanamitindo Hamisa Mobeto alijitabiria kabla hayo hayajatokea.
 

Akistorisha na gazeti hili, Seth alisema Mobeto kwa mara ya kwanza alishiriki katika filamu waliyocheza pamoja kama wahusika wakuu inayokwenda kwa jina la Poor Player ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ambako ndani yake alicheza kila kitu ambacho kimekuja kumtokea.

 

“Yaani Mobeto ni kama alijitabiria mapema maana kabla hajazaa alicheza filamu kama amezaa na mwanaume mwenye mwanamke mwingine kisha akamtelekeza na mtoto kitu ambacho kimemtokea kweli baada ya kuzaa na Mbongo Fleva na kumtelekeza kwa kutotoa matumizi ya mtoto,” alisema Seth.

Advertisements
%d bloggers like this: