Skip to content
Advertisements

Dogo janja afufua ndoto za Harmorapa kwa Wema

Msanii mwenye vituko katoka game ya bongo Harmorapa amempongeza star mwenzake Dogo janja kwa kukamilisha ndoto zake za kumpata Irene Uwoya na kufanikisha kufunga nae ndoa.

Kitendo hiki kimemfanya Harmorapa kupata matumaini mapya juu ya ndoto yake ya kumpata staa wa filamu Wema Sepetu.Akifunguka kupitia ukurasa wake wa instagram Harmorapa aliandika.

“Dah naamini sana katika ndoto kua ipo siku ndoto unayoota itatimia na kua kweli sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera @dogojanjatz naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake….

Nami sivunji imani naamini @wemasepetu ipo siku atakua wangu ugumu alioupata #janjaro umenipa matumaini kikubwa ni kutulia na ndoto yangu na kulenga ipo siku itatimia… One day you will be mine….❤ @wemasepetu”

Advertisements
%d bloggers like this: