Skip to content
Advertisements

Mbwana Samatta nje ya uwanja kwa wiki sita

Mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta na nahodha wa Taifa Stars, atakaa nje kwa wiki sita akiuguza majeraha ya goti. 

Samatta aliumia goti wiki iliyopita wakati akiichezea Genk dhidi ya Lokeren na kulazimika kutolewa nje katika dakika ya 40. 
Lakini leo kutoka Ubelgiji, ameiambia SALEHJEMBE kwamba atatibiwa kwa wiki sita akiwa nje ya uwanja. 
“Baada ya vipimo kutoka, natakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita nikipata matibabu,” alisema. 
Samatta ameonekana kupata maumivu katika goti lake katika misuli na mifupa miepesi ambayo kitaalamu inajulikana kama Meniscus. 
Kuumia kwa Samatta ni pengo kwa Genk lakini pengo pia katika kikosi cha Taifa Stars ambayo yeye ni nahodha.

Advertisements
%d bloggers like this: