Skip to content
Advertisements

SIMU YA ZITTO KABWE YASHIKILIWA NA POLISI

Leo Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto aliripoti Kituo cha Polisi Kamata jijini Dar es salaam kama alivyotakiwa awali na jeshi hilo. Jeshi la Polisi limechukua simu ya ndugu Zitto kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao, na wameahidi kuwa watairudisha kwake kesho jioni, na ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21, 2017. 

Pia Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi yetu “UNASINYAA”. 
Ado Shaibu 

Katibu – Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma 

ACT Wazalendo 

Novemba 7, 2017 

Dar es salaam

Advertisements
%d bloggers like this: