Skip to content
Advertisements

Meek Mill atupwa jela miaka 2-4

Rapper Meek Mill amekumbwa na janga zito ambapo amehukumiwa kifungo cha miaka 2-4 kwenda jela.
Jaji wa Mahakama ya Philadelphia ametoa hukumu hiyo kwa msanii huyo kukiuka masharti ya probation ya kesi yake ya mwaka 2009 ya kumiliki dawa za kulevya na silaha.
Hukumu hiyo imetolewa Jumatatu hii baada ya rapper huyo kupigana kwenye uwanja wa ndege wa St. Louis na kuendesha pikipiki kwa fujo huko mjini New York.
Watu kibao wameonekana kuipinga vikali hukumu hiyo akiwemo rapper jay Z. Kupitia mtandao wake wa facebook Jay ameandika, “The sentence handed down by the Judge — against the recommendation of the Assistant District Attorney and Probation Officer — is unjust and heavy handed. We will always stand by and support Meek Mill, both as he attempts to right this wrongful sentence and then in returning to his musical career.”

Advertisements
%d bloggers like this: