Skip to content
Advertisements

Mlipuko Kagera Tanzania waua wanafunzi sita

Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.

“Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho.” Dokta Mariagoreth ameiambia BBC.

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.

Advertisements
%d bloggers like this: