Skip to content
Advertisements

Marufuku kuitwa ‘Baby”

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amepiga marufuku tabia ya wanafunzi wa kike kuitwa “Baby” kwa madai kuwa ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi.

Tamko hilo amelitoa kwenye ziara yake ya siku moja alipotembelea shule ya sekondari Nasuli iliyopo wilayani Namtumbo, ambapo amekemea tabia hiyo kwa kusema inachochea wasichana kujihusisha na vitendo vya mapenzi wakiwa shule.

“Msikubali kuitwa “Baby” kwasababu kukubali kuitwa “Baby” ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi msikubali kuitwa “Queen” wewe ni mwanafunzi unatafuta maisha”, amesema Mndeme.

Aidha RC Mndeme amewaasa wanafunzi hao kuweka bidii kwenye masomo na kujiepusha na vishawishi ambavyo vinapelekea kupata ujauzito na kulitia hasara taifa ambalo linalipa ada ili wasome bure.

Kwa upande mwingine mkuu huyo wa mkoa amewaonya wanafunzi hao wasijite wazuri kwani hiyo huwafanya wavulana wabaya wawashawishi kufanya mapenzi.

Advertisements
%d bloggers like this: