Skip to content
Advertisements

BREAKING: Mume wa zamani wa Irene Uwoya Ndikumana amefariki, chanzo chatajwa na alichoomba kabla ya kufariki

Asubuhi ya leo Tanzania imezipokea taarifa za kifo cha aliyekuwa Kocha msaidizi wa timu ya Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana Katauti ambae amefariki ghafla.
Mwandishi wa habari za Michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba Gakwaya Olivier ambae ni Afisa Habari wa Timu hiyo amesema Ndikumana amefariki kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.
“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli, bado tunasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu”
Marehemu aliwahi kucheza soka Tanzania akiwa na Stand United na ni Mume wa zamani wa Mwigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja. RIP Ndikumana

Advertisements
%d bloggers like this: