Skip to content
Advertisements

Namibia: Grace Mugabe hayuko hapa

Naibu waziri mku nchini Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, amekana uvumi kuwa nchi yake inamhifadhi mke wa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Grace Mugabe.
“Sijapokea taarifa kama hiyo. Kile ambacho tumejulishwa ni kuwa mke wa rais na familia yake wako salama nchini mwao,” alisema Nandi-Ndaitwah.
Bi Nandi-Ndaitwah ambaye pia anahudumu kama waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, alinukuliwa akisema kuwa yale yanayoendelea katika taifa jirani wao la Zimbabwe yanaleta wasiwasi mkubwa. 

Advertisements
%d bloggers like this: