Skip to content
Advertisements

LADY JAYDEE NA MWANA FA WAINGIA STUDIO PAMOJA 

Wawili hao walikuwa na Ugomvi kwa miaka mingi wameamua kutengeneza ngoma yao ya pamoja. 

Una hamu ya kusikia ngoma mpya kutoka kwa Lady Jaydee na Mwana FA? Basi kiu yako hiyo itakatwa muda sio mrefu.
Wawili hao ambao walikuwa kama Paka na Panya kwa zaidi ya miaka mitano, wameonekana wakiwa kwenye picha ya pamoja katika studio ya B Hitz usiku wa kuamkia Alhamisi hii ambapo wameonekana walikuwa wanatengeneza ngoma yao ya pamoja.
Jide ndio aliyewashtua mashabiki kwenye hilo baada ya kupost picha hiyo katika mtandao wa Instagram na kuandika, “Last night 🎼🎸🎹🎤🎻🎺🥁 #Muziki.”
Jambo hilo linaweza likawa limepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki kwani wawili hao walishawahi kushirikiana katika ngoma kadhaa ambazo ziliteka vichwa vya habari ikiwemo ‘Hawajui’, ‘Msiache Kuongea’, ‘Alikufa kwa Ngoma’ na ‘Wanaume Kama Mabinti’

Advertisements
%d bloggers like this: