Skip to content
Advertisements

Ugonjwa ulioua watu milioni 1.3 watajwa

DAKTARI wa magonjwa ya ndani ya watu wazima katika Hospitali ya Rufani ya Mtakatifu Gaspari iliyopo katika Mji mdogo wa Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida, Dk.Joseph Kazaura amesema zaidi ya watu milioni 1.34 duniani walipoteza maisha kutokana na homa ya ini mwaka 2015.

Dk. Kazaura aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa za hali halisi ya ugonjwa wa homa ya ini katika Hospitali ya Rufani ya Mtakatifu Gaspari katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015/2016 hadi mwaka 2017/2018.
“Hali halisi ya homa ya ini kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mpaka mwaka 2015, homa ya ini ilisababisha vifo zaidi ya milioni 1.34 duniani,” alisema mtaalamu huyo wa afya.
Aidha, Dk. Kazauri alisema idadi kubwa ya vifo vya homa ya ini vilitokea katika nchi zinazoendelea kama Tanzania na kwamba vifo hivyo pia vilisababishwa na maambukizi ya muda mrefu ya homa hiyo inayosababisha ini kunyauka.
Dk. Kazaura alisema kwa mujibu wa takwimu hizo, zaidi ya watu milioni 257 duniani wanaishi na maambukizi ya virusi vinavyosababisha homa ya ini.

Advertisements
%d bloggers like this: