Skip to content
Advertisements

Kocha wa Sevilla akutwa na saratani ya tezi dume

Klabu ya Sevilla imethibitisha kuwa mkufunzi wake amepatikana na ugonjwa wa saratani baada ya timu hiyo kutoka nyuma na kupata sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool.

Vyombo vya habari vinasema kuwa Eduardo Berizzo ambaye anaugua saratani ya tezi dume aliwaelezea wachezaji wake kuhusu habari hiyo katika wakati wa mapumziko katika uwanja wa Estadio Ramon Sanchez Pizjuan.
Wachezaji wa Sevilla walimkimbilia Berizzo baada ya Guido Pizarro kufunga katika dakika za lala salama ili kusawazisha.
Taarifa ya klabu hiyo imemtakia mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 kupona kwa haraka.

Advertisements
%d bloggers like this: