Skip to content
Advertisements

Polisi, Mahakama vinara wa rushwa

Utafiti wa shirika lisilo la kiserikali la Twaweza umebaini kuwa Idara za Polisi na Mahakama bado zinaongoza kwa rushwa, licha ya kuwa ni taasisi zinazohudumia idadi kubwa ya watu. 

Hayo yamebainishwa kwenye uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina “Hawashikiki” uliofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kutoka sekta za umma na kibinafsi.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, wananchi wanaripoti kuwa licha ya viwango vya rushwa kupungua nchini kwa mwaka huu, bado idara za polisi na mahakama zimeendelea kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa ambapo kati ya 36% na 39% ya wananchi waliohojiwa, wameiambia Twaweza kuwa waliombwa rushwa mara ya mwisho walipofika katika taasisi hizo.

Advertisements
%d bloggers like this: