Skip to content
Advertisements

Video:George Stinney mtoto wa kwanza kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa nchini Marekani.

FAHAMU George Stinney ndiye mtoto wa kwanza kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa nchini Marekani. George ambaye alikuwa akitokea kwenye jamii ya watu weusi ambayo ilikuwa ikibaguliwa sana katika eneo la Alcolu huko South Carolina, alituhumiwa kuwaua watoto wawili wa kike wa kizungu na miili yao kuitupa kwenye dimbwi karibu na eneo ambalo alikuwa akiishi. Lakini hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja uliothibitisha kosa hilo, zaidi ya maelezo yaliyoandikwa na polisi aliyemkamata, ambayo pia hayakusainiwa na George. Wakati wa kesi yake George alikuwa akihojiwa bila wazazi wake wala mwanasheria, na wazazi wake hawakuruhusiwa kabisa kumuona, kesi ya George iliandamwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi kwani hata mahakamani hakuna mtu mweusi aliyeruhusiwa kuhudhuria zaidi ya polisi watatu ambao waliokota miili ya hao watoto. Waendesha mashtaka walisema watoto hao walipigwa na kufanyiwa vitendo vya ubakaji lakini ripoti ya daktari haikuonyesha hivyo zaidi ya kueleza walipigwa na kitu chenye ncha kali, na hakukuwa na dalili zozote za kubakwa. Baada ya George kukamatwa baba yake alifukuzwa kazi katika kampuni ya wazungu aliyokuwa akifanya na kuhama katika nyumba aliyokuwa akiishi. George alinyongwa kwa kutumia akiti cha umeme mwaka 1944.

Advertisements
%d bloggers like this: