Skip to content
Advertisements

Wingu Jeusi’ Wema, Mama’ke Kurudi CCM

DAR ES SALAAM: Kutokana na hamahama ya wanasiasa hasa wa upinzani kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa mara nyingine, makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wema Isaac Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu nao wametajwa.
 
Hata hivyo, suala la kutajwa kwao kurejea CCM limetawaliwa na usiri mzito au wingu jeusi. Kwa mujibu wa chanzo makini kinachojadili habari za mastaa wa Kibongo, kuna mkakati kabambe wa kumrejesha Wema na mama’ke chama tawala huku mhusika mkuu wa kufanikisha hilo akitajwa kuwa ni mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

“Ninyi muoneni Steve hivihivi, ndiye anayesuka mpango mzima ndiyo maana uliona juzijuzi alifunguka kimafumbomafumbo kwenye ukurasa wake wa Instagram. “Kama mliona, Steve alianza kwa kumpongeza Albert Msando (wakili aliyehama Chama cha ACT-Wazalendo na kujiunga na CCM) kisha akatoa siri kuhusu dada yetu ambaye ni msanii mwenzao kwamba yupo njiani naye kurudi nyumbani kwa maana ya CCM ambapo Wema alimjibu palepale kwenye posti yake kuwa anaamini anayezungumziwa siyo yeye (Wema) kwani hana mpango huo.

 
“Sasa hapo ndipo ubuyu ulionyooka ukaanza kwamba jamaa anamshawishi sana Wema na mama yake warejee CCM, jambo ambalo linaonekana kuwa gumu kwa wawili hao.
 
“Vyovyote iwavyo, lakini ishu ya Wema na mama yake kushawishiwa kurudi CCM ina usiri mkubwa sana,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kumwagiwa habari hizo katika kipindi hiki ambacho kuna ‘usajili’ wa wanasiasa, jana gazeti hili lilizungumza na Steve juu ya ishu hiyo ambapo mambo yalikuwa hivi;
 
Amani: Mambo vipi Steve?
Kuna taarifa hapa kwamba wewe ndiye unayeinjinia mkakati wa Wema na mama yake kurudi CCM, je, ukweli ni upi?
Steve: Kwanza niseme kwamba, mtoto hawezi kukimbia kwa baba yake milele, ipo siku atarudi tu. Cha msingi ni kuelewa tu kuwa muda utasema.
 
Ni mapema mno kuzungumza chochote, tusubiri muda utafika. Baada ya kumsikia Steve, gazeti hili jana pia lilimtafuta Wema kujua kama ameshavuta ‘fedha za usajili’ ili kurejea CCM ambapo simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumia ujumbe mfupi wa SMS hakujibu.
 
Kwa upande wake, mama Wema alipotafutwa, kama kawaida yake alitoa povu ambalo siyo la nchi hii. “Naomba watu watambue kwamba hakuna tulichosahau CCM na CCM siyo baba wala mama yetu. Sisi hatuna tulichokisahau, tunasonga mbele, tunachokihitaji ni mabadiliko ya kweli,” alisema mama Wema.
 
Februari, mwaka jana, Wema na mama yake walijiunga rasmi na Chadema wakitokea CCM ambapo wawili hao walikaririwa wakisema kuwa, wanakwenda kusaka mabadiliko ya kweli kwenye chama hicho.

Advertisements
%d bloggers like this: