Skip to content
Advertisements

Utapenda Alichokijibu @VanessaMdee Kwa Shabiki Aliyei-Diss Ngoma Yake 

Katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuna ngoma kadhaa kali zimeachiwa na wanamuziki wa Bongo, Vanessa Mdee ni miongoni mwa wanamuziki wa Bongoflava wanaomiliki ngoma mpya mwezi huu.
Bounce yake aliyawakutanisha Maua Sama na Tommy Flavour ndio ngoma ambayo inaufanya upepo wa VeeMoney kuvuma zaidi kwenye masikio ya wapenda burudani ya Muziki.
Kama umeisikiliza Bounce unagundua vionjo ambavyo vimetumika kuikamilisha ngoma hiyo ni vile vilivyosikika kwenye “Bounce Along” ya Wayne Wonder ya mwaka 2003.
Kila mmoja alieisikiliza anajaribu kutoa mtazamo wake juu ya ngoma hiyo akiwemo mtumiaji mmoja wa twitter ambae ameamua kuyasema yale aliyohisi yanastahili kusemwa kama ukosekanaji wa Ubunifu kwenye muziki wa bongo.
Sasa baada ya Vee kukutana na hiyo tweet kwani aliikaushia nae akatoa jibu lake simple tu ambalo kwa kiasi fulani mambo yalikua moto, Tweet ikaenda Viral, Cheki hapa alichojibu.

    Mungu akubariki kwa mchango wako. Hakika umesaidia kujenga taifa 👌🏾 https://t.co/eCM1Np4dhe

    — VeeMoney #Bounce (@VanessaMdee) November 24, 2017

Advertisements
%d bloggers like this: