Skip to content
Advertisements

Chadema wafunguka kuhama kwa wema

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema taarifa za kuhama Kwa msanii maarufu wa filamu nchini, Wema Sepetu wameziona kwenye mitandao ya kijamii gazeti la Mtanzania limeeleza.
Kauli hiyo inafanana na ile ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambako Wema ametangaza kurejea, ambapo Katibu Mwenezi wa chama hicho Humphrey Polepole amenukuliwa akisema hana taarifa hizo.
Ofisa Habari Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema jukwaa alilotumia Wema ni binafsi ambalo Chadema haiwezi kulizungumzia.
“Ule ni ukurasa wake binafsi na ameamua kuandika hivyo hatuna mamlaka ya kuhoji lakini pia kama chama hatujui chochote kuhusu hatua hiyo,” amesema Makene.
Taarifa za kurejea kwa Wema CCM zilianza kusambaa kuanzia saa 12 jioni leo Ijumaa, Desemba Mosi baada ya kuandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa amechoka kuishi kwenge nyumba ya mateso hivyo anarejea nyumbani.

Advertisements
%d bloggers like this: