Skip to content
Advertisements

Wema aitosa chadema na kurudi ccm

Mapema mwaka huu (Februari), msanii huyo alihamia chama cha CHADEMA akidai ameenda kupigania demokrasi ambayo alidai ilikuwa inafifia nchini.
“Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya 

CHADEMA… Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana, kwa sasa I am a proud member of CHADEMA” alinukuliwa Wema Sepetu mara baada ya kuhamia upinzani.
Aidha, msanii huyo anakabiliwa na shtaka la kutumia dawa za kulevya wakili wake akiwa ndg. Alberto Msando ambaye naye katimkia CCM toka ACT-Wazalendo.
Aidha, vipodozi vya msanii huyo (Kiss) vimepigwa marufuku na Serikali kuwa havifai kwa matumizi ya binadamu.

Advertisements
%d bloggers like this: