Skip to content
Advertisements

Polepole aishangaa CUF ‘Chama kina baba wawili’

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitampokea yeyote anayetaka kurudi ndani ya chama hicho bila kufuata utaratibu. Kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni(CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi alizokuwa akizishikilia kwenda CCM.

Polepole aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama.
“Ameamua kule aliko haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina baba wawili huwezi kuwa na nyumba ina baba wawili alafu utasikiliza watoto watamsikiliza nani, basi amehama,” alisema Polepole.
“Sasa mimi niko hapa Musoma mimi nitumie fursa hii anayemuunga mkono ni Rais wetu ambaye ni mwana CCM kwelikweli na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ikimpendeza afuate utaratibu akiona mazuri ya Rais yule asione vinaelea kwa mazuri yale asione vimeshushwa vimeundwa na wanaounda mambo mazuri ya Magufuli ni Chama cha Mapinduzi.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: