Skip to content
Advertisements

Serikali kukabiliana na nguvu za atomiki mipakani

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameiagiza Tume ya Nguvu za Atomiki nchini, kuhakikisha inaweka vituo vya ukaguzi wa viwango vya mionzi kwa bidhaa zote zinazoingia na kutoka nchini katika mipaka yote kwa lengo la kudhibiti mionzi katika bidhaa hizo.
Ametoa agizo hilo jijini Arusha alipotembelea Tume hiyo ili kujionea jinsi inavyofanya kazi, ambapo amesema ni muhimu vituo hivyo kuwekwa katika mipaka ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini zinakuwa na viwango vya mionzi inayokubalika kimataifa.
Ameitaka Tume hiyo kutokuishia katika kutekeleza majukumu ya kudhibiti na kuhamasisha matumizi bora ya mionzi bali inapaswa kuanza kuangalia namna bora ya kuhamasisha matumizi chanya ya nyuklia kwa maendeleo ya taifa katika nyanja za Afya, Kilimo, Maji na Teknolojia.

Hata hivyo, kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki, Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri, amesema kuwa kutokana na upungufu mkubwa wa watumishi walio na weledi katika Teknolojia ya Nuklia imesababisha Taasisi hiyo kukosa watumishi tangu kuanzishwa kwa vituo vya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa katika mipaka ya Rusumo, Mtukula, Kabanga, Kigoma, Tunduma, Kasumulu na Daraja la Mkapa.

Advertisements
%d bloggers like this: