Skip to content
Advertisements

Rayvanny atoa ruhusa kwa yeyote ku-perform ngoma zake jukwaani ila…

Msanii wa muziki Bongo, Rayvanny amesema ni sawa kwa msanii yeyote ku-perform ngoma zake jukwaani ila kuwe na makubaliano.

Muimbaji huyo kutoka label ya WCB ameiambia Daladala Beat, Magic Fm iwapo muhusika amefanya hivyo kutokana na mapenzi yake kwake ni sawa ila show isiwe ya kibiashara na iwapo ni hivyo kuwa na makubaliano maalum.
“Ni ku-appreciate tu kama umependa kazi yake na wewe mwenyewe ni shabiki yake pia” amesema Rayvanny.
“Kama ananipenda ni shabiki yangu aimbe lakini siyo nipo kwenye show kabla sijapanda na yeye aimbe tena nyimbo zangu lakini akijisikia kuimba aimbe lakini siyo biashara analipwa hela anaenda ku-perform ngoma zangu atakuwa ananiibia” amesisitiza.
Hivi karibuni kuliibuka mvutano wa maneno kati ya TID na Ben Pol mara baada ya Ben Pol kuimba sehemu ya wimbo wa TID ‘Nyota Yangu’ katika tamasha la Fiesta, Dar.

Advertisements
%d bloggers like this: