Skip to content
Advertisements

Bendera azikwa akimiminiwa sifa

MAELFU ya waombolezaji kutoka mikoa mbalimbali nchini juzi jioni walishiriki mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Manyara, marehemu Joel Bendera, wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Rais John Magufuli aliwakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo.
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ni miongoni mwa walioshiriki akiwamo pia Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe. Wengine ni wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge, viongozi wa vyama vya siasa na wananchi kutoka mikoa ya Morogoro, Manyara na Dares Salaam.
Ibada ya mazishi iliongozwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga, William Mndolwa, na marehemu alizikwa katika makaburi ya kanisa hilo.
Jafo alisema serikali imepokea kwa majonzi msiba huo na ikizingatiwa Bendera alifanya kazi kwa uadilifu akiwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kisha mkoa wa Manyara.
Jafo alisema Bendera ni miongoni mwa viongozi wachache waliyokuwa na hekima na busara katika kutekeleza majukumu yake na kutumikia nyadhifa kadhaa ndani ya serikali na kwamba kiongozi huyo ni mfano wa pekee katika uchapaji kazi na kuwataka viongozi waliopo madarakani kuiga nyayo za Bendera.
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyet, alisema alikabidhiwa ofisi na Bendera Oktoba 31, mwaka huu baada ya kustaafu Oktoba 26 na kwamba amesikitika sana na kifo cha rafiki yake.

Advertisements
%d bloggers like this: