Skip to content
Advertisements

Mbunge Chadema apingana vikali na Mbowe

Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Anthony Komu ametoa msimamo wake unaotofautiana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuhusu kususia uchaguzi wa majimbo matatu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Mbowe alisema kuwa kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haitaahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika januari 13 mwakani ili kushiriki majadiliano, hawatashiriki uchaguzi huo, lakini Komu amesema kuwa kufanya hivyo ni kosa kubwa ambalo linaweza kuwaathiri katika chaguzi zijazo.

“Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano ya vita, na unatakiwa kuangalia wapi ulipokosea ili ujisahihishe, hata hizo Kata 43 hatukuonewa, ndiyo maana tulipata Kata moja tu ambayo tulijipanga,”amesema Komu

Aidha, Mbunge huyo amesema kuwa uamuzi huo wa kususia uchaguzi unazua maswali mengi, kwani kufanya hivyo kutatoa faida kubwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi katika majimbo yote.

Hata hivyo, juzi Mbowe alisema kuwa kulikuwa na kasoro kubwa katika uchaguzi wa Kata 43, hivyo ni vyema uchaguzi huo wa mwakani ukaahirishwa kupisha mjadala wa wadau wa siasa.

Advertisements
%d bloggers like this: