Skip to content
Advertisements

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba abadilisha muonekano wake


Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amezua gumzo mitandaoni baada ya kubadilisha staili yake ya kufunga nywele kwa nyuma na kunyoa kipara.

Drigba kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa alianza kufunga staili ya nywele zake tangu mwaka 2000 mpaka 2017, lakini kwa sasa ameamua kuwa mpya na kuanza staili nyingine ya kunyoa para.

Mpaka sasa hivi picha hiyo aliyoiweka jana imepata likes, comments na Retweets zaidi ya elfu 1 kwenye mtandao wa Twitter.

Drogba ambaye kwa sasa anakipiga kunako Ligi kuu Soka Marekani katika klabu ya Phoenix Rising FC amekuwa moja ya wachezaji wakukumbukwa katika klabu ya Chelsea kwa muda wote.

Advertisements
%d bloggers like this: