Skip to content
Advertisements

Utata kuhusu kifo cha bilionea na mke wake Canada

Familia ya bilionea raia wa Canada na mke wake wamekosoa ripoti zinazozunguka vifo vya wawili hao.

Polisi wanataja vifo hivyo vya Barry Sherman na mke wake Honey, ambao miili yao ilipatikana kwenye nyumba yao huko Toronto kama vya kutiliwa shaka, lakini wanasema kuwa hakuna mtu anasakwa

Vyombo vya habari nchini Canada vinanukuu ripoti za polisi zikisema kuwa polisi wanachunguza uwezekano wa mauaji na kujiua.

Lakini taarifa ya familia inasema kuwa hakuna mtu anayewafahamu wawili hao anayeweza kuamini hilo.

Miili ya wawili hao ilipatwa na ajenti wao wa nyumba ambaye amekuwa akijaribu kuwauzia nyumba.

Polisi wanasema wanasubiri uchunguzi wa wataalamu wa upasuaji kabla ya kuamua hatua watakazochukua.

Magazeti kadhaa nchini Canada yanasema yaliambiwa kuwa wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa Bw. Sherman alimuua mke wake kabla ya yenye mwenyewe kujiua.

Alikuwa mmoja wa watu matajiri zaidi nchini Canada na aliorodheshwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 3.2.

Advertisements
%d bloggers like this: